Lengo letu katika Matukio ya Kusisimua ya Pili ni kutokeza vitabu na vifaa vingine vya elimu vinavyoongeza uwezo wa watoto wa kutambua masuala ya mazingira duniani na kukuza uwezo wa kusoma na kuandika lugha nyingi.

Nunua Vitabu Sasa (Buy Now)  
Wasomaji Wetu (Our Readers)
Orodha Rasmi ya Usambazaji wa Kitabu (Official Distribution List)
Changia Sasa (Donate Now)

The Adventures of Pili

Tunatokeza vitabu vyenye michoro vinavyotimiza mahitaji ya sasa ya kufundisha watoto walio tayari kukabiliana na changamoto za ulimwengu. Utayari wa kukabili ulimwengu unahusu kuelewa utegemezano na mahusiano, kuzoea utofauti na kuzungumza lugha tofauti na yetu. Kupitia matukio ya kusisimua ulimwenguni kote, vitabu vyetu vinashughulikia masuala ya amani na utayari wa kukabili ulimwengu, tofauti za kitamaduni na uwezeshwaji, ujasiriamali, na utunzaji wa mazingira.

4972721C-897D-4A1B-B6A8-2F47668A9262

Matukio ya Kusisimua ya Pili si tu tafsiri inayowawezesha watoto kujua lugha ya pili. Kutia ndani na michoro mizuri sana, wazazi na waelimishaji watapata kifaa kizuri sana cha kuwasaidia watoto ambao hawajaanza kusoma na ambao wameanza kusoma. Hadithi zetu zimesimuliwa kwa  umakini ili kuhamasisha uwezo wa kusoma lugha mbili kuanzia umri mdogo.

Kwa msaada wako, tunaweza kusambaza mfululizo wa vitabu hivi duniani kote.

PNY-05COLOR

Matukio ya Kusisimua ya Pili ni mradi wa upendo. Sehemu ya mapato yatasaidia kusambaza nakala za bure za vitabu vyetu kwenye jamii zilizo mbali za nchi zinazoendelea. Katika mwaka 2019, tulisambaza nakala 5,000 za bure za vitabu vya lugha mbili kwenye maeneo kama vile katika msitu wa Amazon, Mto Orinoco, na maeneo mengine mengi, unaweza kuona hapa orodha kamili ya usambazaji. Tuko tayari kupokea mawazo na ushirika mwingine. Tafadhali tujulishe. Tungependa kusikia kutoka kwenu.

9ca2d4d6-7909-4953-83e8-008aa1891855

Kwa sasa, michango kwa ajili ya Matukio ya Kusisimua ya Pili inawezesha kupunguziwa kodi na inaweza kupokewa kupitia wadhamini wetu, Kituo cha Safina, shirika la kutoa misaada linalotambulika na IRS kuwa lina msamaha wa kodi chini ya Kifungu 501(c)(3). ****** Hakikisha unataja wazi kuwa mchango wako unaenda kwa Matukio ya Kusisimua ya Pili. ****** Bonyeza hapa ili kuchangia kupitia Paypal au kadi ya mkopo

Unknown-2

Screen Shot 2020-01-21 at 9.13.43 AM

Kike Calvo ni mpiga picha, mwandishi wa habari, na mtunzi aliyewahi kushinda tuzo, ambaye amejikita kwenye utamaduni na mazingira.

Kike ni kati ya watu wa kwanza wanaotumia kifaa chenye kamera kinachopaa angani ili kutokeza picha kwa ajili ya sanaa na kutumiwa kama kifaa cha utafiti na uhifadhi. Ni mwandishi wa vitabu kumi na moja. Mwaka 2018, Kike alianzisha mradi wa “Matukio ya Kusisimua ya Pili” akiwa na lengo la kutokeza vitabu na vifaa vingine vya elimu vitakavyoongeza uwezo wa watoto wa kutambua masuala ya mazingira duniani na kukuza uwezo wa kusoma na kuandika lugha nyingi. Kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya Kiserikali, na kuongezea msaada wa makampuni na wasomaji, kufikia sasa, vitabu 5,000 vya lugha mbili vimetolewa bure kwa watoto wanaoishi kwenye jamii za mbali duniani kote.

PNY-30-31_SQUIRREL_PANO2

Kike ameshiriki safari za kwenye mito za utafiti wa kisayansi huko Kolombia, Brazili, na Peru. Kwa kipindi cha miaka kadhaa, amejiunga na Safari nyingi za National Geographic—kuanzia Uhispania na Patagonia hadi Kosta Rika na Amazon. Pia hufurahia kufundisha katika warsha za upigaji picha na amewahi kuwa mhadhiri aliyealikwa kwenye vyuo vinavyoongoza kama vile School of Visual Arts na Yale University.

 

%d bloggers like this: